OakMfumo wa usimamizi wa hoteli (PMS) Ingia Omba maonyeshoDemo

Vipengele

Kila kitu hoteli inachokitegemea, kwenye mfumo mmoja.

Si vipengele vinavyouzwa kando. Kila kifurushi kwenye ukurasa wa bei kinajumuisha vyote hapo chini — isipokuwa viwili, na tunavitaja: kiunganishi cha njia za mauzo kina bei yake kando, na kufuli za milango zinahitaji vifaa unavyonunua mara moja.

Kila kitu hoteli inachokitegemea

Kila kitu mfumo wa usimamizi wa hoteli unapaswa kufanya, pamoja na sehemu ambazo mingi huiacha. Si vipengele vinavyouzwa kando — kila kifurushi kinajumuisha vyote, isipokuwa kiunganishi cha njia za mauzo, ambacho kina bei yake kando.

Mapokezi na Stay View

Wiki mbili za hoteli nzima, kwenye skrini moja

  • Check-in kwa mbofyoCheck-in, check-out, kuhamisha chumba na kugawa bili.
  • Walk-in na vikundiMalipo ya awali, vikundi na bei za mawakala.
  • Historia ya mgeniTaarifa, vitambulisho na safari zilizopita.
  • Mapokezi au simuInafanya kazi kwenye laptop na kwenye simu.
Stay View ya Oak: kila chumba kwa wiki mbili, kila booking kwa rangi ya ilikotoka, hali ya chumba na ujazo wa kila usiku.
Channel manager

Booking.com, Expedia, Airbnb na channels 100+ zaidi, sambamba

  • Usawazishaji pande mbiliBei na vyumba vinatoka, bookings zinaingia.
  • Masharti ya kukaaKukaa kwa chini, stop-sell, kufunga kuwasili.
  • Rate plansB&B, isiyorudishwa na ya kampuni, kutoka bei moja.
  • Mabadiliko yenyeweKughairi na mabadiliko yanaingia yenyewe.
Kalenda ya bei na upatikanaji ya Oak, ikionyesha bei za usiku na vyumba vilivyopo kwa kila aina.
Booking engine

Ukurasa wako wa bookings, bila kamisheni kabisa

  • Shiriki popoteKiungo cha Instagram, WhatsApp na tovuti yako.
  • Bei za sasa hiviVyumba na bei kutoka kalenda yako.
  • Simu yoyoteMgeni hahitaji kupakua kitu.
  • Moja kwa moja mapokeziInafika kama reservation nyingine, papo hapo.
Ukurasa wa bookings wa hoteli kwenye Oak, ukionyesha jina lake, aina za vyumba na bei kwa shilingi.
Usafi

Wasafishaji na mapokezi hatimaye wanakubaliana

  • Hali ya chumba sasaSafi, chafu, kimekaguliwa au hakitumiki.
  • Kazi zimepangwaVyumba vya kila msafishaji, vilivyochelewa kwanza.
  • Matengenezo na vitu vilivyopoteaVinaandikwa kwenye chumba husika.
  • Kwa KiswahiliKwa watu wanaofanya kazi.
Ubao wa usafi wa Oak, ukionyesha vyumba kwa hali ya usafi na wafanyakazi waliopangiwa.
POS ya mgahawa na baa

Peleka bili kwenye chumba, ipasavyo

  • Huduma ya mezaOda kwa meza, peleka chumbani, funga hesabu.
  • Menyu na vituoVitu, nyongeza na bei kwa kila kituo.
  • Kugawa na kufutaVyote vinaonekana kwenye ripoti.
POS ya Oak, ikionyesha meza kwa kila kituo — baa, bwawa na mgahawa.
Back office na hesabu

Sehemu mifumo mingi ya hoteli inaiacha kwa Excel

  • Kufunga hesabuMatumizi, ukasha na hesabu ya droo kwa zamu.
  • Bili za makampuniAkaunti za kampuni na ankara.
  • Kamisheni na bajetiMawakala, wauzaji, wamiliki wa vyumba na bajeti.
  • Kila njia ya malipoM-Pesa, Mixx, Airtel, HaloPesa, AzamPesa, kadi, taslimu, benki.
Back office ya Oak, yenye matumizi, kufunga fedha, ukasha, kampuni, kamisheni, ankara na bajeti.
Night audit

Funga siku kwa dakika, si jioni nzima

  • Siku kwa mtazamo mmojaUjazo, gharama na fedha zilizokusanywa.
  • Hakuna kinachopoteaBili zisizolipwa na wasiofika kabla tarehe haijasogea.
  • Muhtasari wa ukashaKwa njia ya malipo, na gharama kwa aina.
  • Chapisha au PDFNakala ya kumbukumbu, kila usiku.
Night audit ya Oak: ujazo, gharama zilizopelekwa, malipo yaliyokusanywa na folio ambazo hazijalipwa.
Ripoti

Takwimu mmiliki anazoziuliza kweli

  • Ujazo, ADR, RevPARKwa siku, mwezi na aina ya chumba.
  • Bookings zinatoka wapiKila OTA, moja kwa moja, mawakala na walk-in.
  • Nani anadaiwaDeni la wageni, wadaiwa, amana na wasiofika.
  • Kwa mhasibu wakoKila kitu kinatolewa kwa mbofyo mmoja.
Skrini ya ripoti ya Oak, ikionyesha ujazo, mapato na wastani wa bei kwa kipindi.
Door locks

Msimbo upo mlangoni kabla mgeni hajafika

  • Kila mlango, kalenda mojaVyumba, lango la bwawa, ofisi.
  • Namba pamoja na bookingZinatolewa na kuondolewa zenyewe.
  • Nani alifungua niniKila ufunguaji unaandikwa, na kila namba iliyokataliwa.
  • Matatizo kwanzaBetri iliyoisha au kufuli lisilo mtandaoni linaonekana mapema.

Inafanya kazi na kufuli za kidijitali za TTLock. Wewe ununue kufuli na lango la mtandao; Oak hufanya mengine. Tuulize nasi tutaangalia milango yako pamoja nawe.

Kalenda ya kufuli za milango ya Oak: kila mlango upande, wiki mbili zijazo juu, na mgeni ambaye msimbo wake upo hai kwenye kila mlango kila usiku.

Iione ikifanya kazi kwa hoteli yako

Dakika ishirini, kwa simu au ana kwa ana. Lete orodha ya vyumba na bei zako, na utaiona hoteli yako ndani ya Oak kabla hatujamaliza.

Omba maonyesho ya dakika 20

Au piga simu +255 748 113 305.